Top Stories

Mbowe, Viongozi CHADEMA kulala Mahabusu hadi April 3

on

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru Viongozi 6 wa CHADEMA akiwemo Freeman Mbowe, wafikishwe mahakamani hapo April 3,2018 ili kukamilisha masharti ya dhamana yao.

“Nikitoa dhamana wakati washtakiwa hawapo haina maana zoezi zima lisimame.” -Hakimu 

“Leo washtakiwa hawajafikishwa mahakamani na nimetoa masharti ya dhamana, hivyo kutoa dhamana na washtakiwa wakiwa bado hawajasaini ilo zoezi bado halijakamilika.” -Hakimu 

“Hivyo kwenye hatua ya sasa ni mapema mno kwa upande wa mashtaka kuwasilisha hoja za kukata rufaa wakati bado mchakato haujakamilika.” -Hakimu

“Mahakama inatoa remove order waje mahakamani April 3,2018 na wadhamini wao ili waje kukamilisha masharti ya dhamana.” -Hakimu

BREAKING: Mbowe, Viongozi Watano CHADEMA wapewa masharti ya dhamana

Soma na hizi

Tupia Comments