Matukio ya wazazi kunyanyasa watoto tena hata wa kuwazaa wenyewe bado yameendelea kutokea kila wakati sehemu mbalimbali duniani.
Huko Nigeria kuna stori inamuhusu baba mmoja..eti kaamu kukata vidole vya mwanae wa kumzaa kisa tu kaiba nyama bila kumwomba mama yake ruhusa ya kuchukua.
Hata hivyo polisi hawakumuachia baba huyo aitwaye Surulere Rafael kwa kumfungulia mashtaka na alipoulizwa sababu ya kumkata mwanaye huyo alisema alimwibia fedha kiasi cha zaidi ya 10,000 za Kitanzania pia aliiba mboga bila kuomba na kuamua kumpa adhabu hiyo.
Kwa sasa mtoto huyo amelazwa hospitali huku akiendelea kupatiwa matibabu wakati baba yake akiendelea kushikiliwa na polisi.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.