Kocha wa Manchester United Louis van Gaal alijiunga na klabu ya Man United toka mwaka 2014 akichukua mikoba ya David Moyes aliyetimuliwa kazi. Imeripotiwa kuwa Van Gaal sio kocha rafiki na wachezaji, kitu kilichopelekea kumkosa Pedro Rodriguez.
September 10 stori iliyofichuka ni kuwa Louis van Gaal aligombana na wachezaji toka msimu wa Ligi Kuu haujaanza, stori kutoka mtandao mirror.co.uk unaeleza kuwa kikubwa kilichopelekea Van Gaal kupishana na wachezaji wake, ni aina ya mfumo anaotumia kuwasliliana na wachezaji sio rafiki, hivyo kujikuta akigombana na wachezaji kutokana na ukali wake.
Stori inasema kuwa wakati timu ipo Marekani kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, Van Gaal aliwakataza wachezaji kutembea, wala kufanya kitu chochote kwa madai kuwa kilichowapeleka ni maandalizi ya msimu na sio kingine chochote. Hivyo wachezaji wakawa na ratiba ya kula, kufanya mazoezi na kulala.
Kocha Louis van Gaal sio rafiki wa wachezaji inadaiwa mastaa wengi wa klabu hiyo wamewahi kutofautiana na kocha huyo. Wachambuzi wa masuala ya soka wanasema kwa ushirikiano huu ni ngumu kupata mafanikio akiwa na wachezaji ambao hana mahusiano nao mazuri. Di Maria amewahi kukiri moja kati ya sababu zilizomfanya ahame Man United ni Van Gaal.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos