Tarehe kama ya leo Mexico iliingia kwenye headlines baada ya kuwepo na taarifa ya kupotea kwa wanafunzi 43 katika mji wa Iguala Kusini mwa nchi hiyo.
Pamoja na kuwepo utata wa kupotea kwa wanafunzi hao huku ndugu wa wanafunzi hao wakigoma kupokea taarifa ya Serikali iliyotolewa baada ya uchunguzi uliodai wanafunzi hao walitekwa na kuuawa na kundi la kigaidi.
Ripoti hiyo haijakataliwa tu na ndugu wa wanafunzi hao, bali pia ripoti kutoka kwa kundi la wataalamu wa uchunguzi hivi karibuni ilihoji uhalali wa ripoti hiyo ya uchunguzi wa serikali.
Ndugu wa wanafunzi hao wamesisitiza kuwa hawataacha kuandamana hadi pale watakapojua ukweli juu ya ndugu zao hao.
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, ameahidi uchunguzi upya ufanywe.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE