Polisi Mkoani Mwanza wanamshikilia Mganga wa Kienyeji Hemed Jumanne (40) Mkazi wa Sengerema kwa tuhuma za kumbaka mgonjwa wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Jumanne Muliro amesema Mganga huyo anadaiwa kutenda kosa hilo baada ya Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 32 kwenda kwake kupata tiba ndipo akapata tamaa za Kimapenzi na kumpa dawa za kumpumbaza kisha kumuingilia kimwili.
“Mganga huyo alijipaka dawa kwenye uume wake na kuuingiza kwenye sehemu za siri za Mwanamke huyo akidai anampa matibabu, huu ni ukatili wa kinyama, tutamfikisha Mahakamani “ -RPC Mwanza