Leo August 20, 2018 Kwa mara ya Kwanza Wananchi wa Korea Kusini wameingia Korea Kaskazini kukutana na ndugu zao tangu kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha nchi hizo mbili kugawanyika.
Kwa kipindi cha takribani miongo 6 iliyopita mipaka ya nchi hizo mbili ilifungwa na familia kutengana.
Wazee 89 wakiwa wenye furaha wameingia Korea Kaskazini leo kwaajili ya kukutana na ndugu zao waliotengana.
Tukio hili ni matokeo ya vikao vya kidiplomasia vilivyofanyika baina ya viongozi wa nchi hizo mbili.