Mbunge wa Kawe ambaye pia ni Msemaji wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya Fedha na Mipango, Halima Mdee alisimama Bungeni leo November 6, 2018 na kuwasilisha maoni ya mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka wa fedha 2019/20 ambapo amelieleza Bunge kuhusu athari zinazoweza kujitokeza nchini kufuatia matukio ya utekaji na mauaji yanayoendelea kujitokeza mara kwa mara.
“Baadhi ya wafadhili wameanza kukataa kutoa fedha kutokana na mwenendo wa siasa za nchi yetu usioridhisha, Kambi rasmi ya upinzani Bungeni pamoja na watanzania wote tunalaani na tunapinga vitendo viovu vya ukandamizaji, utekaji na mauaji” –Halima Mdee