Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Temeke imezungumzia jinsi ilivyoshinda kesi ya rushwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni kutoka kwa Mjasiriamali Mwajuma Abdallah aliyemshawishi Askari kupokea rushwa ili kumuachia mtoto wake.
Akizungumzia ushindi wa kesi hiyo namba 75 ya mwaka 2019, Mkuu wa TAKUKURU Temeke, Donasian Kessy alisema Mama huyo alimshawishi na kutoa rushwa kwa
Askari Polisi wa Kigamboni, Hamis Ramdhan ili amsaidie kumtoa mtoto wake rumande aliyeshikiliwa kwa kosa la wizi wa kutumia silaha.
“Mahakama ilimkuta na hatiani Mama huyu na alipewa adhabu ya kulipa faini ya Laki Mbili ama kifungo cha miaka mwili gerezani, pia Takukuru inaendelea na kesi nyingine 9 mahakamani,”.