Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Makanisa zaidi ya 15 yamekutwa yamelaza Wagonjwa kwa mwaka mmoja bila kwenda Hospitali huku ndani ya Makanisa hayo kukiwa na Matunguri sambamba na Waumini kupigwa Viboko wakati wa kuombewa Mkoani Kagera.
Mkuu wa Wilaya Karagwe Godfrey Mheruka ameamua kuingilia kati suala hilo baada ya kufanya msako.