Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Rapper Asap Rocky anaweza kaa jela miaka 6, kisa ugomvi (+Video)

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Rapper Asap Rocky amejiingiza kwenye vurugu pamoja na timu yake na kuanza kupigana na shabiki mmoja ambaye mpaka sasa hajafahamika jina kwenye mitaa ya Stockholm nchini Sweden.

Mtandao huo umeachia baadhi ya video zikimuonyesha Rapper huyo akipigana huku chanzo cha ugomvi kikitajwa kuwa shabiki huyo alidai kuharibiwa headphones zake na Asap na kudaiwa kuwa jamaa huyo alimuita rapper huyo nyuma ya mgahawa waliokuwepo na kuanza kupigana. 

Inaelezwa kuwa Polisi wa Stockholm wamemshikilia Asap Rocky na wanaweza fanya hivyo kwa siku tatu au kulipa dhamana kutokana na kilichotokea au vinginevyo kufungwa kabisa jela miaka 6 nchini humo na tayari mpaka sasa watu watatu wamekamatwa kwa tuhuma zilizotokea.

PART ONE: HIKI NDICHO KISIWA CHA MSILA WANAFUNZI HUTUMIA MITUMBWI KUVUKA ZIWA KWENDA SHULE

Soma na hizi

Tupia Comments