Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya habari zilizoandikwa kwenye magazeti ni hii kwenye gazeti la Majira yenye kichwa cha habari ‘Mgodi mwingine wa dhahabu kujengwa Sengerema’
#MAJIRA Mgodi mwingine wa dhahabu kujengwa Sengerema utatumia bil 30.8 kukiwa na hazina ya wakiwa mil 2.8 za dhahabu pic.twitter.com/qZQw97DyFJ
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
Gazeti hilo limeripoti kuwa mgodi mwingine wa dhahabu unatarajiwa kufunguliwa katika kijiji cha Sota, kata ya Igalula wilayani Sengerema mkoani Mwanza baada ya kampuni ya OreCorp Tanzania Ltd kwa kushirikiana na ile ya ACACIA kukamilisha utafiti wake kijijini humo.
Mgodi huo utatumia bilioni 30.8 kukiwa na hazina ya wakia milioni 2.8 za dhahabu, ambapo ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwakani, jambo ambalo limeelezwa litasaidia kuinua uchumi wa wananchi waishio wilayanin humo na taifa kwa ujumla.
Meneja utafiti wa Kampuni hiyo amesema kuwa utafiti huo ulianza mwaka 1999, lakini ulichelewa kuanza kutokana na kampuni kupokezana umiliki, ambapo wao wameingia ubia na kuanza kazi hapo tangu oktober mwaka jana na wanatarajia kukamilisha utafiti wa mwisho mwaka 2017.
Amesema mgodi huo utajengwa mara baada ya kuridhika kuwa matokeo ya utafiti ya waliowatangulia ya kuwepo kwa akiba ya wakili milioni 2.8 ya dhahabu katika eneo hilo yatakuwa sahihi.
#MWANANCHI Rais Magufuli aeleza alivyokuwa akilala usiku wa manane kuchambua majina 185 ya wakurugenzi wa wilaya pic.twitter.com/iAoMk33nUh
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#MWANANCHI Watu watatu wanaosadikiwa kuwa vinara wa kutengeneza vyeti bandia na nyaraka za serikali wakamatwa Dar pic.twitter.com/iuSTZ7Z01m
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#MWANANCHI Mwalimu mkoani Mara anusurika kufa kwa kucharangwa mapanga kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi pic.twitter.com/Fil39NPrmJ
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#MWANANCHI Aliyetajwa na JPM kuwa amekuwa akiibia serikali mil 7 kwa dakika asomewa mashtaka 199 pic.twitter.com/HfdsCjTXwN
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#MWANANCHI Mahakama ya rufani yafufua kesi ya ubunge wa Bulaya, yaamuru isikilizwe upya na mahakama kuu Mwanza pic.twitter.com/eed7CIyA8k
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#MTANZANIA JPM afichua namna mtandao ktk ofisi ya TAMISEMI ulivyokuwa ukipokea hongo kwa ajili ya nafasi za uteuzi pic.twitter.com/qmNJTWIYIo
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#JamboLEO Rais wa Uganda, Yoweri Museveni asimamisha msafara wake wa magari ili apokee simu faraghani pic.twitter.com/vpEqQ3MCTi
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#JamboLEO Kiongozi wa upinzani Uganda, Besigye ambaye amezuiliwa kwa wiki kadhaa, amepewa dhamana na mahakama kuu pic.twitter.com/SjIpFcXEmI
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#JamboLEO Mkurugenzi mkuu TCAA, Hamza Johari amesema rada iliyofungwa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere imezeeka pic.twitter.com/rBRk8KNmpE
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#HabariLEO Rais Magufuli asema wakurugenzi aliowateua hakuwachagua kwa kubahatisha wala hakuchagua vilaza pic.twitter.com/vDYIV9M5EE
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#HabariLEO Serikali imelazimika kusitisha ajira mpya 71,496 hadi pale tatizo la watumishi hewa litakapopata ufumbuzi pic.twitter.com/2QxgNyQ9uK
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#HabariLEO Polisi 200 waanza doria Dodoma kwa lengo la kujiweka sawa kukabiliana na vurugu zozote zitakazojitokeza pic.twitter.com/9P7lLvKpjo
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#HabariLEO Viongozi BAVICHA wapandishwa kizimbani Dom wakikabiliwa na mashtaka ya kukutwa na maandishi ya uchochezi pic.twitter.com/nVbWlXEWwg
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#NIPASHE Rais Magufuli amewapa maagizo saba wakurugenzi likiwamo la upatikanaji wa madawati na utunzaji wake pic.twitter.com/gOB1xlWDr8
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#NIPASHE Serikali yaagiza kufanyika kwa uhakiki vyeti vya taaluma kwa watumishi wa umma ili kubaini wenye vyeti feki pic.twitter.com/ZHuuUrMNlA
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#MWANANCHI Waziri Muhongo aahidi kuwa ifikapo 2030 kila nyumba kuwasha umeme nchini pic.twitter.com/cWOrvkBwvQ
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#MWANANCHI Ugunduzi mpya wa nyayo za viumbe wa kale eneo la Laetoli Hifadhi ya Ngorongoro kuchangia kuongeza watalii pic.twitter.com/DYFFD1y7db
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#MWANANCHI Hali ya utulivu imerejea Sudan Kusini baada ya Rais Salva Kiir kuagiza wanajeshi watiifu kusitisha vita pic.twitter.com/RyE301U9NG
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#NIPASHE Hekari 37,000 za misitu huteketezwa kila mwaka kwa ajili ya matumizi ya nishati ikiwamo kuchoma mkaa pic.twitter.com/MfqGLKJF5M
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#NIPASHE Rais Shein asema serikali yake ina uhakika wa fedha kutokana na kumudu kufikia malengo ya makusanyo ya kodi pic.twitter.com/XEPpRXYpLn
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#NIPASHE Tanzania kutouza meno ya tembo yaliyokamatwa kwa kuhofia kuchochea biashara haramu ya ujangili pic.twitter.com/Kw1mb5YrNC
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#MWANANCHI Azam Media imeongeza udhamini wake ligi kuu bara msimu ujao ili kuongeza ushindani kwa timu shiriki pic.twitter.com/xqSix5F7vn
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#LeteRAHA Kocha wa Simba, Omog amesema anahitaji mwezi mmoja wa kuinoa timu hiyo ili kupata kikosi imara pic.twitter.com/5FC685aar0
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
#CHAMPIONI Uongozi simba umepeleka barua TFF inayoonyesha inataka kulipwa mil 126 ili Kessy aanze kuichezea Yanga pic.twitter.com/nKUQpRgOEC
— millardayo (@millardayo) July 13, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 13 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI