Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Muttamwega Mgaywa amesema akichaguliwa Serikali yake itaongeza idadi ya ndege kufikia 50 na atahakikisha kila Mtanzania anakuwa na ajira ya uhakika.
Akizindua kampeni zake katika eneo la Kituo cha Mabasi Mombasa Jijini DSM, Mgaywa amesema sera za chama hicho zimejikita katika kutatua kero za wananchi hususan kero ya ukosefu wa ajira.
Amesema kuwa, Chama Chake kikipata idhini ya kuiongoza Tanzania, Serikali yake itawapa mikopo wakulima ambayo italipwa baada ya wakulima kuvuna na kuuza mazao yao.
Vipaumbele vingine ni huduma ya maji safi na salama bure, elimu mpaka Chuo bure, matibabu bure na ameahidi kuwa itakuwa Serikali ya Kilimo na Viwanda, aidha, atamteua Ummy Mwalimu na Kassim Majaliwa kuwa Mawaziri.