Leo March 12, 2020 Mwanaume mmoja kutoka London, Uingereza, amethithitishwa kuwa ndiye mtu wa pili kupona Virusi vya HIV vinavyosababisha UKIMWI, wamesema Madaktari.
Adam Castillejo bado hajapatikana na Virusi baada ya kukaa siku 30 bila kumeza dawa za kupunguza makali ya Virusi vya HIV zinazofahamika kama Anti-retroviral.
Madaktari walieleza kuwa hakupona kutokana na dawa za HIV, bali kwa tiba ya uboreshaji wa seli alizopewa kwa ajili ya matibabu ya saratani ambayo alikua nayo, limeripoti jarida la kitabibu la The Lancet linaloandika juu ya HIV.
Watoaji wa seli hizo wana geni zisizo za kawaida ambazo walimpa Castillejo, ambazo zilikuwa kwa ajili ya ulinzi dhidi ya HIV.
Mwaka 2011, Timothy Brown, “mgonjwa Berlin ” alikua ni mtu wa kwanza kuripotiwa kuwa amepona HIV, miaka mitatu na nusu iliyopita baada ya kupata tiba sawa na hiyo.