Leo December 19, 2017 Katibu Mtendaji wa Baraza la SUMATRA Dr. Oscar Kikoyo ameeleza kuwa kulingana na kanuni mpya za SUMATRA za mwaka huu, vitendo vya kupiga miziki isiyoendana na maadili ya Kitanzania, kuhubiri siasa na kufanya biashara ndani ya mabasi vimepigwa marufuku.
Ameomba abiria kuonesha ushirikiano kwa SUMATRA na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa endapo vitendo hivi vitaendelea kwenye mabasi ya mikoani.
Ameeleza pia kuwa kwenye kanuni hizi za mwaka 2017, watu wenye ulemavu wakatae kulipa pesa ya ziada kwa ajili ya vifaa vinavyowasaidia kutembea kama magongo, wheelchair na vinginevyo.
Vitu alivyozungumza RC Mghwira alipofika chuo anachofundisha