Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM Lazaro Mambosasa amepiga marufuku waendesha pikipiki maarufu kama (bodaboda) kuingia katikati ya Jiji la DSM kuanzia kesho Agosti 6 2019 mpaka hapo mkutano wa nchi za kusini mwa Afrika (SADC) utakapoisha.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mambosasa amesema “Katika kipindi hiki cha mkutano wa SADC Jeshi la polisi kanda maalum DSM linapiga marufuku pikipiki (Bodaboda )zote kuingia/kufika maeno yote ya katikati ya Jiji kuanzia August 06 hadi August 18,2019, Kutokana baadhi ya bodaboda kujihusisha na vitendo vya uhalifu” Mambosasa
“Polisi inapiga marufuku kuweka taa za vimulimuli au za rangi rangi, taa zenye mwanga mkali (spot light) na kufunga ving’ora kwenye magari ya kiraia au watu binafsi na pikipiki za kiraia, isipokuwa magari yanayotoa huduma za dharura tu na ya makampuni binafsi ya ulinzi” Mambosasa