Leo July 3, 2018 tunayo story kutokea kwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ambapo amesema serikali inatumia takribani Sh. Bilioni 269 kwa ajili ya kununua dawa kutoka nje ya nchi.
Akizungumza wakati wa mkutano na Kampuni ya Madawa ya Fosunpharma, Mwijage amesema viwanda vya dawa za binadamu ni miongoni mwa bidhaa zinazotumika sana.
Amesema miongoni mwa sehemu ambazo hawajafanya vizuri ni katika sekta ya mafuta ya kula na upande wa dawa za binadamu.
“Katika mchakato huu wa uchumi wa viwanda tumesema hakuna kikwazo kuhusu kampuni hiyo kuwekeza katika Madawa ya Binadamu,” amesema Mwijage
RAIS MAGUFULI ‘NIMECHOKA KUTUMA RAMBIRAMBI’