Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemuondoa madarakani Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO), Charles Bukombe kwa kosa la kuyapuuza maagizo yake na kuyaita ya kisiasa.
Licha ya kumuondoa katika nafasi hiyo, Waziri Lugola amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake, kumchukulia hatua kali za kinidhamu RTO huyo ili iwe fundisho kwa matrafiki hao wa mikoa nchini.
Lugola amesema RTO huyo ameshuhudia katika video ambayo ilikua inasambaa mitandaoni akiwa katika mkutano jijini Arusha, akipinga maagizo yake na kuyaita ya kisiasa na pia kutokuyatekeleza.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa Mji wa Malinyi, Mkoani Morogoro, leo, Lugola amesema yeye hatoi maagizo ya kisiasa bali anatoa maagizo yatakayomsaidia rais kazi zake kwa wananchi wanyonge wanaopambana na umaskini na ajira.
“Namuagiza Katibu Mkuu achukue hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kumuondoa u-RTO afanye shughuli zingine za kipolisi na maRTO ambao mkono wangu haujafika kwenu, wengine nimeanza kuwaona hamsimamii vizuri maagizo yangu, wapo ambao wanaendelea na uonevu, wapo baadhi ya askari wanaendelea kuchukua rushwa barabarani,” Lugola.
“NILIAMBIWA SIWEZI ILA LEO MIMI NDIO MBUNGE” HALIMA BULEMBO