Kumekuwa na kejeli katika mitandao ya kijamii juu ya muonekano wa Wahudumu wa Shirika la ndege la Tanzania kitu ambacho hakijamfurahisha Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe.
Zitto kupitia Facebook akaunti yake ameandika hivi na nukuu “Dada zetu wanaofanya kazi Shirika letu la ndege wamekuwa wakifanywa kichekesho mtandaoni. Hawa ni Wanawake Watanzania wenzetu wapo kazini. Kusambaza picha zao na kuwacheka sio uungwana na ni ukandamizwaji kijinsia.”
“Sijapenda na naomba Watanzania wenzangu tuache. Tujivunie vyetu ikiwemo raia wetu kama hawa. Kama unawapenda waethiopia au Wakenya kwenye ndege zao, hamia huko. Kuwasakama dada zetu wanaofanya kazi ATCL ni umazwazwa. Tumepewa na Mungu hawa, tuwape moyo.” Zitto Kabwe
Mwandosya akataa kuchangia ada ya Mtoto, ataka iundwe kamati ya Ada/harusi
RAIS MAGUFULI AMTUMA MSTAAFU KIKWETE ZIMBABWE, CHEYO NAE