Mkuu wa Wilaya Handeni Godwin Gondwe amesema Serikali haitamvumilia Mtu yeyote atakayekuwa kikwazo kwa mtoto wa kike kupata elimu iwe kwa kumpa mimba au kumkataza kuhudhuria masomo shuleni atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Gondwe ameyasema hayo wakati wa uchimbaji wa msingi kwaajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya Sekondari Kwamatuku iliyopo katika Wilaya yake.
Aidha Gondwe amewataka Wazazi kuwa makini na watoto wao katika kusimamia maendeleo yao pindi warudipo nyumbani kutoka mashuleni ili kujua changamoto zinazo wakabili na waweze kuzitatua kwa haraka.
MEYA SELEBOSS “‘WADADA WANAOJIUZA’ TWENDENI SHAMBANI KWANGU”, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA