Serikali imekanusha taarifa taarifa zilizosambaa zikieleza kuwa serikali ya Tanzania imemfukuza balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Roeland van de Geer.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga ambapo ameweka wazi kuwa balozi huyo hajafukuzwa kama inavyoelezwa bali ameitwa makao makuu ya umoja huo.
”Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania, Roeland van de Geer anayetarajia kuondoka leo usiku kwenda makao makuu ya EU hajafukuzwa bali ameitwa na umoja huo kikazi” Waziri Dk. Mahiga.