RC Makonda ameunda kamati maalum ya watu 17 itakayoshughulika na masuala ya mapenzi ya jinsia moja jijini DSM kwa kile alichokieleza ni kukomesha biashara hiyo ndani ya Mkoa wa DSM.
Kamati hiyo itashughulika na waigizaji wa filamu za ngono nchini, wamiliki wa nyumba zinazotumika kuigiza video za ngono, pamoja kuwatafuta watu wanaotumia mitandao kutapeli.
“Tumefikiria tuunde kamati, kamati itakayokuwa kwenye makundi manne, moja itakayojihusisha na kundi lote la mashoga, wanaojitangaza na wale wasiojitangaza lakini wanajulikana ni mashoga na nimeshapata taarifa nyumba takribani 24 wanazofanyia kazi, wanachukua wakina dada, wanawanywesha madawa na kuwafanyia vitendo hivyo wakiwarekodi” –RC Makonda
Makonda amezitaka mamlaka zinazohusika na haki za binadamu nchini kutoingilia suala hilo kwa kile alichokisema suala hilo ni kinyume na taratibu na sheria za Tanzania.
“Ndugu zangu wa haki za binadamu nafahamu hili jambo nilishawahi kuligusa kipindi cha nyuma, na mataifa mengine ambayo mataifa yao yamepokea na kukubali ushoga, sisi tuna utamaduni wetu, tuna sheria zetu, msituingilie” RC Makonda