Baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumkuta na kesi ya kujibu aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF), Jamal Malinzi na wenzake wawili katika mashitaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha wakatikiwa kuanza kujitetea.
Malinzi ndio amekuwa mtu wa Kwanza kuanza kujitetea mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama ya Kisutu, Maira Kasonde, huku akiongozwa na Wakili wake Richard Rweyongeza.
Malinzi ambaye alisisima kwenye kizimba cha mahakama chenye urefu wa unaoweza kuwa wa futi 3 hadi 4, alianza kujitetea kwa kuelezea wasifu wake.
Malinzi ameeleza kuwa alikamatwa Juni 27, 2019 siku ya Jumanne saa 8 mchana ambapo wakati huo akiwa ni Mfanyabiashara wa Kampuni ya Cargo Star.
Pia alikuwa ni Rais wa TFF, pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Kagera .
Baada ya kueleza hayo, Malinzi anatarajia kuendelea na ushahidi wake wa kujitetea Agosti 15, 2019.