Leo June 23,2018 tunayo story kutokea kwa Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Hospital ya Agha Khan, Dk. Aleesha Adatia ambapo anasema ugonjwa wa saratani ni wa familia nzima na sio mgonjwa peke yake.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dk. Adatia anasema endapo mgonjwa wa saratani akipata matatizo basi familia nzima itahusika kwa sababu ndio inamuhudumia.
“Ndio maana tunatoa elimu kwa familia na mgonjwa ili tuwasaidie kwa sababu mgonjwa akiangaika hata familia itaangaika, hivyo sio ugonjwa wa mtu mmoja,”– Dk. Adatia
Dk. Aditia amesema ugonjwa wa saratani sio mwisho wa maisha bali mgonjwa anahitaji ukaribu wa familia ili aweze kujisikia faraja kama watu wengine.
“Ndio maana tunawakutanisha pamoja ili wasijisikie wapweke bali wajione kama watu wengine, tuwaleta pamoja ili wabadilishane mawazo na wanakuwa na furaha kwa sababu inawasaidia sana,” amesema.