Leo August 3,2018 tunayo story kutoka Jeshi la Polisi Kanda Maluum ya Dar es salaam ambapo linawashikilia watu 2 kwa tuhuma za kuteka watu na kudai fedha.
Watuhumiwa hao ni Hussein Shilingi (30) mkazi wa Kimara Mwisho na Martin Pumba (35) makazi wa Tabata.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, SACP Lázaro Mambosasa amesema watu hao walitiwa mbaroni July 26, 2018 maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM).
Kamanda Mambosasa amesema watuhumiwa hao walikuwa wakitumia gari yenye namba za Umoja wa mataifa (UN) ambazo ni T 452 CD 639 Toyota Land Cruiser huku ndani ya gari hilo wakiwa na watu 5 waliowateka.
“Baada ya kufanya upekuzi ndani ya gari hilo tulifanikiwa kukamata vifaa vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu hao ambavyo ni, redio call moja, pingu jozi tatu, plate namba za magari za mashirika ya serikali,”
JOKATE: “kwa vyovyote vile sitotoa siri nitazozijua kwenye Ukuu wa Wilaya”