Leo June 24, 2018 kuna hii ya kuifahamu Mahakama ya jinai nchini Maldives imemhukumu aliyekuwa rais wa nchi hiyo Maumoon Abdul Gayoom kifungo cha miezi 19 gerezani kwa kosa la kuzuia utekelezaji wa sheria.
Mahakama hiyo pia imemhukumu Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Maldives Abdulla Saeed na Jaji Abdullah Yameen kifungo cha miezi 19 kwa kosa hilohilo.
Watu hao walipokamatwa na polisi, walikataa kukabidhi simu zao. Gayoom amesema idara ya uendesha mashtaka haiwezi kuthibitisha kuwa upo ushahidi wa kutosha kwenye simu zao.
Habari nyingine zinasema, watatu hao bado wanakabiliwa na kesi ya uhalifu wa kupindua serikali.
MAGAZETI LIVE: Tishio Jipya, Rais, Waziri Mkuu Walipuliwa kwa Bomu