Nusu ya mshahara wa Rais Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa utatumika kwa ajili ya kuendeleza miradi ya kijamii nchini humo.
Rais Ramaphosa ametangaza hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kusema fedha hizo zitakwenda kwenye mfuko maalum unaosimamiwa na Wakfu wa Nelson Mandela .
Japo bado haijafahamika ni mshahara kiasi gani anapokea kwa mwezi, japo vyombo vya habari vinadai anapokea zaidi ya Dola elfu 20 alizokuwa akilipwa Jacob Zuma.
Afrika Kusini na dunia kwa ujumla mwaka huu inaadhimisha miaka 100 tangu kuzaliwa kwa kiongozi wa kwanza mzalendo wa taifa hilo Marehemu Nelson Mandela, kwa kutayarisha matukio mbalimbali ya kijamii.
Baba wa kijana anayedaiwa kufufuka amezungumza ‘Mtu mwingine atakufa”