Leo July 2, 2018 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amefanya ziara katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa DSM Mwananyamala na kutoa maagizo mbalimbali kwa watumishi wa hospitali hiyo.
Miongoni mwa agizo alilotoa Waziri Ummy Mwalimu ni ujenzi wa ghorofa mbili kwa ajili ya wodi ya wazazi ambapo kwasasa wajawazito 6 wanalala katika kitanda kimoja.
Waziri Ummy pia ametangaza rasmi kuwa hospitali zote za rufaa za mikoa kuanzia jana July 1, 2018 zipo chini ya wizara hiyo ambapo kabla ya maamuzi hayo zilikuwa chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Kitaa (TAMISEMI).
Tangazo hilo la Ummy Mwalimu ni kufuatia agizo la Rais Magufuli alilolitoa November 25, 2017 akiwa katika uzinduzi wa hospitali ya taaluma na tiba ya Mloganzila.