Mwili wa Mwanajeshi mmoja, vijana 10 wa JKT na Wafanyakazi wawili wa basi la Igunga Express waliofariki June 14 mwaka huu katika eneo la maili tano mtaa wa Igodima Mbeya itaagwa kesho katika kambi ya JKT Itende
Akizungumza na waandishi wa Habari leo June 18, 2018 katika ukumbi wa JKT Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Jeshi la Wananchi (JWTZ ) Kanali Ramadhan Dogoli amesema taratibu zote zimekamilika.
Amesema taratibu zote zitafanyika kambini hapo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Jeshi na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mbeya.
Aidha Kanali Dogoli amesema chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa na mamlaka husika ambapo taarifa itatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.
Hata hivyo amewaomba Wananchi jijini Mbeya kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia tukio la kuagwa miili hiyo ambapo baada ya kuagwa miili itasafirishwa kwenda maeneo mbalimbali nchini.
Majeruhi wameendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa Mbeya, JKT Itende na Hospitali ya Jeshi Mbalizi.
CHADEMA wazungumza Mbowe kuanguka ghafla, kulazwa (+video)