DCB Commercial Bank imekua ya kwanza kuzindua huduma mpya za simu ya mkononi Mjini Dodoma. Kwa sasa kupitia DCB Digital mteja ataweza kufungua akaunti ya muda maalum( Digital FDR), kudunduliza amana kwa malengo maalum(Kibubu Digital Account), Kuchukua mshahara mapema (Digital Salary Advance) na kutoa pesa kwenye ATM za umoja zilizopo zaidi ya 250 nchi nzima bila ya kutumia ATM card (Digital cardless ATM) huduma zote hizi zinapatikama kupitia *150*85# au DCB Digital App kwenye play store.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Mgeni Rasmi Naibu waziri wa Fedha na Mipango Dk Ashatu Kijaji na Viongozi mbalimbali wa Serikali Mizengo Kayanza Pinda Waziri Mkuu Mstaafu, Josephat Kandege Naibu waziri wa Tamisemi, Wabunge mbalimbali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Patrobas Katambi Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini, Richard Wambali Mkurugenzi wa Benki Kuu Tawi la Dodoma, Wateja wa DCB na wageni waalikwa.