WWF Tanzania chini ya mwavuli wa mradi wake wa maji safi wakishirikiana na Wizara ya Maji na Umwagiliaji (MoWI) kupitia Kikundi kazi cha Ufundi (TWG1) chini ya Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP) wanafanya warsha ya siku mbili kuanzia Morogoro ili kuwezesha Jumuiya za watumiaji wa maji kubadilishana mawazo na kutafuta namna rahisi ya kutatua changomoto zinazowakabili katika kushughulikia tatizo hili.
Akifungua warsha hiyo, Praxeda Paul Kalugendo, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali za maji, sehemu ya utunzaji wa vyanzo vya maji- Wizara ya Maji (MoWi), amesema “Wizara inajua umuhimu wa usimamizi sahihi wa rasilimali za maji na tunasaidia sana katika kazi uhamasishaji na utekelezaji wa majukumu ya jumuiya za watumiaji wa maji-WUAs.”
“Kwa uwakilishi wangu hapa ninatarajia kuona sisi sote tutimize malengo ya mkutano huu kama ilivyopangwa (pamoja na WLG na WEM) kuja na masuala yatakayowezesha utatuzi wa changamoto mnazokumbana nazo katika kuisaidia serikali katika jukumu lake la msingi la kuhakikisha maji yanakuwepo kwa matumizi ya vizazi vya sasa na baadae.” -Praxeda Kalugendo
Ameongeza kuwa, Mageuzi ya usimamizi wa rasili za maji nchini Tanzania yamesababishwa na Sera ya Maji ya Taifa ya mwaka 2002 (NAWAPO), Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP ) 2006-2015, Sheria ya Usimamizi wa Maji Nambari 11, 2009 na Sheria ya Utoaji Maji na Usafi wa Maji No.12 ya 2009.
Aidha, mfumo mpya wa taasisi umetokea kama matokeo ya mageuzi ambayo yanashirikisha ushiriki wa watumiaji wa maji mbele katika usimamizi wa rasilimali za maji. Inatarajiwa kuwa ushiriki wa watumiaji wa maji utaleta ufanisi ambao pia utaimarisha uwajibikaji na kufanya maamuzi kwa karibu na watu na kuhakikisha kuwa mipangilio, mazingira ya vipaumbele na utoaji wa huduma kuendana na mahitaji ya ndani.
Kwa upande wake mratibu wa mradi wa maji baridi WWF (Fresh Water programme), Christian Chonya, ameelezea malengo ya warsha hiyo kuwa ni:
“Kuwa na mjadala wa wazi juu ya changamoto wanazokumbana nazo Jumuiya za watumiaji wa maji (WUAs) ikiwemo masuala ya kisiasa, ambapo wanasiasa huwazuia WUAs kufanya shughuli zao ili kulinda wapiga kura wao.”
Chonya ameongeza kuwa, WWF inaamini jamii ikishirikishwa moja kwa moja katika uhifadhi wa vyanzo vya maji, itakuwa rahisi mno kwa vyanzo vilivyo hatarini kukauka na vilivyokwisha kukauka kulindwa na kuendelea kuhakikisha usalama wake hasa kwa vile ambavyo vipo karibu na jamii na hata ambavyo vipo mbali na jamii kwanza kwa kuwawezesha kupima ardhi yao na kuwapangia matumizi bora ya ardhi.
Kwa upande wake Evagris Makfura, msimamizi wa mradi wa maji baridi ofisi ya Iringa, amesema kuwa;
“Kama ilivyo lengo la awali la mradi, shirika la uhifhdi wa mazingira duniani WWF ofisi ya Tanzania kupitia wataalamu wake imeona ni vyema kuwa na mjadala wa wazi ambao unawashirikisha wadau wote wa jumuiya za watumia maji ambao utatoka na makubaliano ya namna gani WUAs watafanya shughuli zao na kuleta hamasa za uhifadhi kwa jamii na mamlaka zote kujua umuhimu wa shughuli za WUAs”
“Wadau hawanabudi kufahamu kuwa, maji ya mito hii inapita mbugani na yanategemewa na wanyama, mazingira pamoja na viumbe vingine na hivyo kukosekana maji kuna madhara makubwa kuliko watu wanavyoweza kudhani.”
Aidha, Makfura alisitiza mchango mkubwa uliyofanywa na WWF katika kuwashirikisha wadau na wananchi kwa ujumla katika suala zima la utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji ikiwa ni pomoja na kushirikiana na Ofisi ya Maji Bonde la Rufiji katika kuunda jumuiya za watumia maji.
Akichangia kwa upande wao, Rajabu Juma kadege, Mwenyekiti wa Jumuiya ya watumia maji bonde dogo la mto Lyandembera Mufindi Mkoani Iringa (LYAMUF).
Amepongeza sana mpango ulionziswa na taasisi ya Tanzania National Park (TANAPA) kwa kushirikiana na wadau wengine kuanzisha na kutoa tuzo katika jumuiya za watumia maji kwani tuzo hizo zimeweza kwa kiasi kikubwa kuleta mafanikio ya kuwahamasisha na kuwapa uwezo ili jumuiya ziweze kufanya kazi zao za uhifadhi vizuri.
“Kutokana na tuzo hii na fedha tunazopata imetufanya mara nyingi tuwe tunapitia na kuviboresha vyanzo maji ili tuweze kushinda mwaka unaofata, kwa mfano jumuiya yetu inatunza vyanzo vya maji 217 lakini vyanzo 50 kati ya hivyo vimeboreshwa vikiwemo, vyanzo vya Lyambungu, Muvengi, Kinego na vingine vingi ambavyo vinamwaga maji yake katika mto Lyandembere na pia chanzo cha Balari, ambao mto huo unamwaga maji yake katik Mto Ruaha Mkuu (The Great Ruaha).”
Mwaka 2017 tulishiriki kwenye Tuzo ya TANAPA na tukaibuka washindi wa kwanza na hivyo takepewa sh million 2 za ushindi na kwa maamuzi ya wajumbe kwenye kikao chetu tuliazimia kujenga ofisi ya jumuiya yetu, hivyo tukaanza mchakato wa kununua ardhi na tukaipata na hata sasa tunaendelea kujenga na kufikia karibu na kufunga renta na tunatarajia tuzo ya mwakani tutashinda na kupata fedha za kumalizia ujenzi wetu.”
Programu ya maji safi ya WWF kwa ufadhili kutoka WWF Sweden imeandaa warsha hii ikiwa na lengo la kuwezesha kuwajengea uwezo jumuiya za watumia maji (WUAs) hasa katika maeneo ya kukusanya taarifa, usimamizi na ushirikishwaji wa jamii pamoja na kuanzisha mjadala wa kupitia miongozo ya uansishwaji na uendeshaji wa shughuli za Jumuiya.
Praxeda Paul Kalugendo, akifungua warsha ya kubadilishana uzoefu kwa jumuiya za watumia maji kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali za maji sehemu ya Usimamizi na utunzaji wa vyanzo vya Maji- Wizara ya Maji na Umwagiliaji (MoWi) tarehe 11/09/2018 mjini Morogoro.
Evagris Makfura, msimamizi wa mradi wa maji baridi ofisi ya Iringa, akitoa maleezo ya jinsi WWF ilivyoshirikisha wadau katika shughuli za uhifadhi wa mazingira katika ukanda wa mto Ruaha Mkuu (The Great Ruaha River).
Mratibu wa mradi wa maji baridi WWF (Fresh Water programme), Bw. Christian Chonya, akiwaelezea washiriki walio kaa kwenye makundi namna ya kuzitambua na kuchambua changamoto wanazokumbana nazo Jumuiya za watumiaji wa maji (WUAs) ikiwemo masuala ya kisiasa, ambapo wanasiasa huwazuia WUAs kufanya shughuli zao ili kulinda wapiga kura wao.
Rehema Omindo, Afisa maji wa Bonde la Wami Ruvu, akielezea ushirikiano unaohitajika baina ya wafanyakazi wa idara za mabonde na jumuiya za watumia maji ili kuongeza ufanisi wao katika utendaji kazi na pia anaeleza juu ya umuhimu wa ushirikiano baina ya Bonde na WUAs kusaidia kuhamasisha jamii kulinda na kuvitunza vyanzo vya maji.
Richard Laizer, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Bonde dogo la Ngarenanyuki lililopo wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, akichangia moja ya mafaniko ya jumuiya yao ambayo kwa asilimia kubwa kwa kuanzisha sheria ndogo ndogo ambapo zinatamka wazi kwamba mwananchi yeyote akisogelea chanzo cha maji kufanya shughuli yeyote ya kibinaadamu ikiwa ni pamoja na kukata majani, miti au kulima mazao, adhabu yake atakamatwa na kulipa tozo ya laki 5 papo hapo.
LIVE MAGAZETI: JPM aagiza TAKUKURU ifumuliwe, Makontena ya Makonda yatinga Bungeni