Mwandishi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) Azory Gwanda ambaye amepotea katika mazingira ya kutatanisha tangu Novemba 21,2018 na mpaka sasa hajulikani alipo ameshinda tuzo ya Daudi Mwangosi inayotolewa kila mwaka na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).
Mwenyekiti wa Jopo la Majaji wa Tuzo ya Mwangosi Mwaka 2018, Ndimara Tegambwage amemtangaza Azory Gwanda kuwa mshindi wa tuzo hiyo wakati wa mkutano mkuu wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania UTPC unaofanyika katika ukumbi wa Lush Garden Hotel jijini Arusha.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mtanzania Absalom Kibanda amekabidhi tuzo hiyo kwa mke wa Azory Gwanda (Anna Pinuni) ambaye hajulikani alipo tangu Novemba 21,2017.
LIVE MAGAZETI: JPM ashtukia msamaha wa Kodi, Pigo la mwisho kwa Makonda