Leo December 12, 2018 Mkurugenzi wa Health Promotion Tanzania Dr. Peter Bujari kwa niaba ya Asasi za Kiraia zinazojishughulisha na ‘Afya kwa wote’ amsema Watanzania 66 katika kila mia hawana bima ya afya na hivyo wanahitajika kulipia huduma pindi wanapougua.
Dr Bujari amesema mpango mkakati wa kugharamia afya ulioundwa mwaka 2015 uliazimia kuunda mfuko wa bima ya afya kwa wote na mfuko mmoja wa kuwekeza fedha kwa ajili ya afya ili kuondoa matumizi makubwa.
Ameendelea kusema kuwa Bajeti ya Sekta ya Afya sio tu ni nusu ya mahitaji bali hata zinazotolewa huwa ni pungufu ya bajeti iliyotengwa.
HUYU NI WAZIRI KANGI LUGOLA KATIKA UBORA WAKE, BONYEZA PLAY HAOA CHINI KUMTAZAMA