Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa mwezi wa kumi na mbili mwaka huu anatarajia kuhamia rasmi makao makuu ya nchi Dodoma kama ilivyokuwa matamanio ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Rais Magufuli “Azimio la Arusha ukilisoma unajua kila kitu kuhusu nchi yetu, baba wa taifa mwaka 1973 alisema tuhamie Dodoma ndio makao makuu ya nchi, Dodoma tunahamia na mimi ndio nakaribia kumalizia, mwezi wa 12 nihamie huko.”
“Niwaombe watanzania wenzetu tuendelee kuitunza amani yetu, maana hatuna baba mwingine wakutusimamia zaidi ya baba wa mbinguni, lakini kifo cha baba wa taifa kitufunze watanzania tuwe na mshikamano, na kila mmoja tuendelee kumuombea huko aliko aendelee kupumzika kwa amani, ameongeza Rais Magufuli.