Mahakama Kuu Kanda ya Moshi imetupilia mbali maombi ya Werandumi Ulomi mdogo wa Bilionea Jubleti Ulomi ya kusimamia na kukusanya mali za Bilionea huyo na kuwapa haki hiyo watu watatu Mjane Zainab Rashid na Mtoto wa Marehemu Julius Ulomi na Werandumi.
Akisoma hukumu hiyo Msajili wa Mahakama Frank Maimbari kwa niaba ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi Dr. Fauz Twalib na kusema Mahakama hiyo imetupa maombi hayo kwa maslahi ya kulinda pande zote hasa Watoto wa Marehemu.
Jaji Twaib amedai awali Werandumi aliyekuwa akitetewa na Wakili Joseph Ngiloi aliwasilisha maombi ya kutaka kuwa msimamizi wa muda wa mali za Marehemu lakini alipingwa na Mjane Zainabu Rajab aliyezaa watoto wawili na Bilionea huyo na mtoto mwingine wa Marehemu Julius Jublet.
Amesema kwa kifungu cha 23 cha Sheria ya Mirathi kutokana na maamuzi hayo hakuna chochote ambacho kitafanyika juu ya mali za Bilionea huyo ambaye alikuwa akimiliki migodi Mirerani, nyumba mashamba na mali kadhaa bila makubaliano ya pande zote.
Mahakama imewatahadharisha pande zote na kuwataka kukaa pamoja na kutoka na mawazo ya pamoja wakiongozana na Mawakili wao na endapo itaonekana hakuna maelewano sheria inaweza kuamuru awepo msimamizi mmoja.
RAIS MAGUFULI ALIVYOONDOKA NAMIBIA NA KUPOKELEWA ZIMBABWE NA RAIS MNANGAGWA