Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imemwandikia barua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kubadili sheria na kumuwezesha kila mtu kujipima UKIMWI nyumbani.
Hayo yamesemwa leo May 31, 2018 na Waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mtambulie(CUF), Masoud Abdalla Salim aliyetaka kujua mkakati wa ziada wa Serikali wa kutambua wanaopata athari za ugonjwa huo.
Waziri Mwalimu amesema maambukizi yameongezeka kwa Dodoma kutoka asilimia 2.4 hadi asilimia 5 sawa na Tanga na Mwanza na kuwa utafiti maalumu unafanyika kubaini chanzo cha kupanda kwa maambukizi hayo.
Kuhusu dawa za Virusi vya UKIMWI (VVU), Waziri Mwalimu amesema zipo kwa asilimia 100.
Mashine za EFD hazifanyi kazi nchi nzima, Serikali yakiri