Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amesema Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka ndie Mkuu wa Mkoa anaeongoza wa kufanya kazi vizuri kuliko wote Tanzania ni kwa mujibu wa ripoti aliyonayo.
“Wakati nateua wakuu wa mikoa na wilaya, vyombo vyangu viliniambia kuwa Anthony Mtaka hafai hata kuwa U-DC. Mimi nikaamua kumpa U-RC, saivi MA-RC gani wanafanya vizuri, ripoti zinaonesha namba 1 ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka.” -Rais Dkt Magufuli