Maafisa wa wanyama pori wamesambaza picha za nyoka mwenye macho matatu aliyepatikana katikati ya barabara kaskazini mwa Australia. Shirika la huduma kwa wanyamapori na bustani za wanyama Northern Territory Parks and Wildlife Service wameeleza kwamba nyoka huyo ambaye picha zake zilisambaa katika mitando ya kijamii ni wa “kustaajabisha”.
.
Amepewa jina la Monty Python nyoka huyo aina ya chatu alifariki wiki kadhaa tu baada ya kugunduliwa Machi. Wataalamu wanasema jicho la tatu la nyoka huyo lililo juu ya kichwa chake limeonekana kuwa ni mabadiliko ya asili.
Maafisa walimgundua nyoka huyo katika mji wa Humpty Doo, 40KM Kusini Mashariki mwa Darwin. Ana urefu wa inchi 15 na alikuwa akipata tabu kula chakula kutokana na ulemavu wake.
MPISHI MKUU WA SIMBA AFUNGUKA CHAKULA WANACHOKULA WACHEZAJI WA SIMBA ILI WABEBE UBINGWA