Leo August 24, 2018 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete amekanusha kutoa ujumbe uliokuwa unasambaa kwenye mitandao ya kijamii kwa kupost video katika akaunti yake ya Instagram yenye caption isemayo. “Ikumbukwe Watanzania wenzangu na ususani WanaCCM wenzangu, mapema mwanzoni mwa Mwaka huu 2018, tarehe 22 niliutaarifu umma ukweli juu ya kile nilichokiita maneno ya kiuchonganisha yanayolenga kunigombanisha Mimi na Uongozi wa Chama changu CCM.”
“Kupitia ujumbe mdogo wa Video nilikanusha juu ya maneno hayo kwamba sikuyaandika mimi na wala sina uhusiano wowote na maneno hayo. Lakini la kushangaza baada ya miezi Saba, jambo hilo linaibuka tena leo.”-Ridhiwani
Aliedelea kuandika Ridhiwani “Nimeweka video niliyoirusha tarehe 22 January Usiku huo nikielezea kutofurahishwa kwangu na kitendo hicho kilichofanyika. Sijawahi sema wala kuandika maneno hayo, yanayolenga kukiambia Chama na Serikali yangu kupuuza hawa wanaohamia chama na kupelekea kufanyika chaguzi za mara kwa mara”
“Nataka kuwahakikishia, kama Mwanasheria ninatambua Haki aliyonayo Raia kikatiba. Sintokuwa tayari kusema neno ambalo litapotosha kiapo Changu kama Mwanasheria ninayeheshimu Haki na Usawa katika Binadamu.”-Ridhiwani
“Ndugu Watanzania wenzangu napenda kuwahakikishia kuwa sihusiki na Maneno hayo na Ninawaomba sana muyapuuze.” amehitimisha Ridhiwani
BALAAA NA NI HATARI: Wagandana wakifanya mapenzi, aliewanasisha aeleza alivyofanya