Upelelezi wa kesi ya mauaji inayomkabili Mfanyabiashara Hamis Said (38), anayetuhumiwa kumuua Mkewe Naomi Marijani upo katika hatua za mwisho kukamilika katika Mahakama ya Kisutu.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amemueleza Hakimu Mkazi, Salum Ally kuwa upelelezi wa kesi hiyo upo katika hatua nzuri na za mwisho kukamilika.
Wakili Wankyo ameomba shauri hilo liahirishwe hadi tarehe nyingine ambapo kesi imeahirishwa hadi Oktoba 7, 2019 kwa ajili ya kutajwa.
Mshitakiwa anakabiliwa na kosa la mauaji ambapo anadaiwa kumuua Mke wake Naomi kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake.