Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea kielelezo cha Kamera ya kurekodia video na tepu mbili kwa ajili ya kutumika katika ushahidi wa kesi ya uchochezi inayowakabili Viongozi 9 wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe.
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kupitia hoja za pande zote mbili.
Hakimu Simba amesema kuwa Kifungu cha 18 cha sheria ya ushahidi wa kieletroniki kimeweka vigezo vya upokeaji wa vielelezo vya eletroniki ambavyo shahidi namba sita Koplo Charles alikidhi.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 26, 2019 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.
UMEMALIZA KIDATO CHA NNE AU SITA NA UPO ARUSHA HII NI HABARI NJEMA KWAKO