Beki wa zamani wa club za Man City, Aston Villa na timu ya taifa ya England Micah Richard ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka baada ya kucheza kwa mafanikio katika vilabu mbalimbali.
Micah Richard mwenye umri wa miaka 31 amelazimika kutundika daruga kucheza soka kutokana na kuwa na jeraha sugu la goti ambalo limekuwa likimuweka nje mara kwa mara hiyo ni kwa mujibu wa rafiki zake wa Man City.
Beki huyo hadi anatangaza kustaafu kucheza soka alikuwa amepitia katika kituo cha kukulia vipaji cha Leeds na baadae Oldham na baadae Man City akiwa na umri wa miaka 14 wakati huo na miaka mitatu baadae kucheza mchezo wake wa kwanza katika 175 aliyowahi kuichezea Man City.
Wakati Richards anaanza kuichezea England mchezo wake wa kwanza wa kimataifa dhidi ya Uholanzi November 2006 aliweka rekodi wa kuwa beki mdogo kuwahi kuchezea England baada ya Rio Ferdinand.