Meneja wa aliyekuwa mfalme wa Pop duniani Michel Jackson alijaribu kumteka staa huyo kumuokoa kutokana na dawa za kulevya.
Meneja huyo Ron Weisner ambaye ndiye aliyekuwa akidhibiti taaluma na kipaji cha marehemu Michael tangu enzi za ujana wake alikuja na mpango wa kutaka kumuokoa mfalme huyo wa Pop katika kilele cha matatizo yake mwaka 2006 wakati aliporipotiwa kuanza kuathiriwa na dawa alizokuwa akitumia.
Kwa mujibu wa wataalamu kutoka kitabu kipya cha Ron kiitwacho ‘Listen Out Loud’, Meneja huyo alipanga kujiingiza katika mpango huo na dada wa Michel, Toya Jackson kumrubuni staa huyo wa ‘Thriller’ wamuibe na kumpeleka Rehab.
Licha ya kujadili mpango huo mara 10 kwa mwaka mzima, La Toya alimuomba Ron kuachana na mpango huo katika dakika za mwisho.
Ron ameweka wazi kuwa aliguswa kufanya hivyo kwakuwa alimuona Michael akiwa si mwenye afya nzuri na kuwa katika hatua nyingine akimfananisha kama mtu aliyekuwa vitani ambapo alimuonea huruma sana.