Michezo

Mipango mipya ya Dani Alves kuhusu klabu yake ya Barcelona!!

on

alveMlinzi wa pembeni wa Barcelona Dani Alves amekataa ofa ya kuongezewa mkataba na klabu hiyo kwa ajili ya msimu ujao na wakala wake tayari amethibitisha hilo.

Alves ambaye amekaa ndani ya klabu hiyo kwa miaka saba huku akiwa amekisaidia kikosi hicho kutwaa mataji mbalimbali amekataa ofa mpya na kusema hajawa tayari kuongeza mkataba na klabu hiyo.

alvesWakala wake Dinorah Santana ambaye alikuwa mke wake wa zamani alisema mteja wake amekataa ofa nyingine na klabu hiyo ya kuongezewa mkataba wa miaka mingine mitatu.

Beki huyo wa zamani wa Sevilla amekuwa akihusishwa kuhamia Manchester United,Manchester City zote za England pamoja na PSG ya Ufaransa.

millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments