Michezo

Taarifa ya kilichomkuta mcheza mieleka wa Mexico ikufikie mtu wangu…(Video)

on

agueroMchezo wa mieleka umeonekana kuwa mchezao hatari pengine kuliko michezo yote licha ya kujizolea umaarufu mkubwa na kupendwa na watu wengi duniani.

Taarifa ikufikikie mtu wangu kuhusu mtoto wa mcheza mieleka maarufu wa Mexico aitaye Hijo del Perro Aguayo ambaye amepoteza maisha wakati alipodondoka jukwani akiwa katikati ya mchezo ikiwa ni saa chache baada ya kukimbizwa hospitali.

Mwanamieleka huyo alikuwa akipigana na mwezake Rey Mysterio katika pambano lililofanyika ijumaa usiku na mara baada ya kudondoka alikimbizwa hospitali lakini madaktari walithibitisha kuwa tayari amefariki.

Wakati akiwa amedondoka chini wenzake hawakujua kiasi gani ameumia na kuendelea na mchezo na baada ya dakika zipatazo mbili waligundua kuwa amezidiwa hivyo kumuwahisha hospitali.

Hapa kuna video ikionyesha wakati pambano hilo linafanyika hadi mwana mieleka huyo alipopoteza  fahamu akiwa ulingoni.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments