Kwa mara ya kwanza Watanzania wamechaguliwa kuwa sehemu ya Kamati ya Scouts Afrika ambapo Mkutano Mkuu ulifanyika Nairobi, Kenya Agosti 25 hadi 28, 2022.
Akizungumza na Ayo TV na Millardayo.com Yasin Othman ambaye ni Mshiriki wa Mkutano Mkuu wa Afrika amesema nchi zilizoshiriki ni takribani 39 ambapo nchi 4 tu ndio zinatakiwa katika kamati hiyo.
“Miongoni mwa ajenda ilikuwa ni kupitia mabadiliko ya Katiba, kupitia mpango kazi wa miaka 3, pia ajenda ya Uchaguzi ambapo tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na Wizara ya Mambo ya Nje ilitusaidia kuwaambia Mabalozi watupigie kura na sasa Tanzania tumeshinda,” amesema.