Kwa wale wakazi wa magorofani au wanaokwenda na watoto wao kwenye nyumba hizi zenye urefu kwenda juu inabidi waichukue hii kama tahadhari manake ni hatari nyingine kwa yeyote.
Madaktari wa watoto wanasema mara nyingi watoto wanapoanguka kwenye umbali kama huu huwa hawaponi na hata wakibakiwa na uhai bado akili zao zinakua zimepata majeraha kwa kiasi kikubwa.
Pamoja na hiyo sentensi ya Madaktari, mtoto Musa Dayib mwenye umri wa mwaka mmoja ameanguka kutoka kwenye kibaraza cha gorofa ya 11 huko Minneapolis Marekani lakini amebakiwa na uhai wake japo hali yake sio nzuri na anapumua kwa msaada wa mashine.
Amevunjika mikono, mgongoni ambapo daktari mwingine wa watoto amesema Watoto wako flexible na huwa hawavunjiki hawaumii haraka kama watu wazima.
Kaa karibu na mimi kupitia Twitter kwa kubonyeza HAPA, pia Instagram na Facebook kwa kubonyeza INSTA na FB ili kila stori inayonifikia niitume kwako iwe usiku au mchana.