Hatua ya makundi ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa mwaka 2017 maarufu kama AFCON 2017 imemmalizika kwa usiku wa January 24 kuchezwa michezo miwili ya Kundi D ya kukamilisha ratiba ya hatua ya Makundi.
Kundi D lilikuwa na timu za Ghana, Mali, Misri na Uganda lakini kabla ya michezo ya leo kuchezwa Misri na Ghana walikuwa tayari wamefuzu kucheza hatua ya robo fainali ila tu mchezo wa leo ulikuwa ni wakukamilisha ratiba na kujua kati ya Ghana na Misri nani atapata nafasi ya kuongoza Kundi D.
Kwa mara nyingine tena Mohamed Salah aliyetoa pasi ya kuiondoa Uganda katika michuano ya AFCON 2017, ndio amekuwa hatari kwa Ghana baada ya dakika ya 11 kuifunga Ghana goli kwa mkwaju wa faulo, goli ambalo lilidumu kwa dakika zote 90 za mchezo 1-0 na kuifanya Misri ipate nafasi ya kumaliza kileleni mwa Kundi D.
https://youtu.be/7x-MZ5uCC7Q
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4