Kuna wakati niliwahi kuhisi kwamba huenda huku kwetu Afrika tunavunja rekodi nyingi sana ila hazipati nafasi kusikika duniani kote kwa sababu nyingi, moja ni ishu ya kutokuwa na utaratibu mzuri wa kuhifadhi kumbukumbu.
Jamii zetu zamani hazikuwa na utaratibu mzuri wa utaratibu huo kwa vile vitu kama vyeti vya kuzaliwa havikuwepo, wenzetu walikuwa na utaratibu mzuri miaka mingi iliyopita hivyo waliweza hata kuitambua siku, tarehe na mwaka aliozaliwa Misao Okawa, ambaye alikuwa kwenye kumbukumbu za Kitabu cha Guiness.
Rekodi zilizomuingiza Misao Okawa kwenye kitabu hicho mwaka 2013 ni ile ya mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani pamoja na rekodi ya mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi duniani.
Misao Okawa amefariki akiwa na umri wa miaka 117, kumbukumbu zinaonesha alizaliwa March 5 1898, ameacha watoto watatu na wajukuu wanne.
Wakati wa birthday yake mwaka huu alisema siri ya kuishi muda mrefu ni ratiba yake ya kulala kwa saa nane kila siku na kula sushi, chakula alichokipenda zaidi.