Najua watanzania na waafrika wote walikuwa wanahamu ya kufahamu mshindi wa Miss World 2016 atakuwa ni mrembo kutoka nchi gani, mashindano hayo ambayo yamefanyika Washington Marekani, Afrika ilipata nafasi ya nchi za Kenya na Ghana kuingia TOP 20.
Muda ulifika na waandaaji wa Miss World walitangaza mshindi ambapo Miss Puerto Rico ndio alifanikiwa kushinda taji la Miss World 2016, lakini muwakilishi wa Tanzania Diana Edward kwa bahati mbaya hakufanikiwa kufika nafasi za juu.
Hata hivyo Afrika Mashariki imepokea good news baada ya nchi ya Kenya kufanikiwa kuingia TOP 5 na ndio nchi pekee ya Afrika iliyofanikiwa kuingia TOP 5, huku Miss Dominician Republic akishika nafasi ya pili na Miss Indonesia akishika nafasi ya tatu.
VIDEO: Miss Honduras na Miss Mexico wameipata ‘Muziki’ ya Darassa wakiwa Marekani