Hatimaye kinyang’anyiro cha kumsaka Redds Miss Iringa kinatarajia kufanyika Juni 20 mwaka huu baada ya aliyekuwa mratibu wa kwanza Mohamed Mcholeka kutoweka katika mazingira ya kutatanisha na kushindwa kufanyika Juni 6 kama yalivyopangwa.
Shindano la Redds Miss Iringa limekuwa chachu ya ajira kwa mabinti wengi kwa kuweza kutangaza vipaji vya washiriki wanaojitokeza kushiriki kila mwaka.
Hadi sasa warembo 12 wamejitokeza kushiriki shindano hilo na wanaendelea na mazoezi katika ukumbi wa Hotel ya Gentle hill kwa mujibu wa Ripota wa nguvu Deniss Mlowe.
Ungependa stori kama hizi zisikupite na zikufikie wakati wowote? niko tayari kukutumia wakati wowote iwapo utajiunga na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.